Friday 26 December 2014

SHEMEJI NA MIPAKA YAKE YA KISHERIA NDANI YA UISLAMU


Kila sifa njema zinamstahikia Allah (subhanahu wa ta‘ala) Muumba wa kila kilichomo katika ulimwengu huu. Swala na salamu zimuendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allahu alaihi wa sallam).

Shemeji huwa ni ndugu wa kiume wa mume kwa mke au ni ndugu wa mke kwa mume. Watu hutumia neno shemeji katika kuonesha uhusiano uliokuwepo baina yao. Lakini leo hebu tuangalie ni yapi yanayofanywa ndani ya jamii za kiislamu baina watu na shemeji zao na uharamu wake ndani ya uislamu.

Kwanza tambua ewe ndugu yangu mpenzi kuwa shemeji yako si mahaarim yako(anaweza kukuoa au unaweza kumuoa). Wako watu hudhani kuwa shemeji yake hana neno. Hayo ni makosa lazima sheria za kiislamu zichungwe wakati wa kukaa nae.

Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam)“Tahadharini na kuingia kwa wanawake(kuingia majumbani mwao)”. Akaulizwa: “Je, ndugu wa mume [shemeji])”. Akasema (Swalla Allahu alayhi wasallam): “Huyo (shemeji) ni mauti” (Bukhari na Muslim).

Miongoni mwa mambo yasiyofaa kufanywa mbele ya shemeji na jamii zetu wanajisahau nayo:

1-Kutovaa hijabu ya kisheria. Wako baadhi ya waislamu wanadhani kuwa mbele ya shemeji yake anaweza kuvaa vyovyote. Kwa mfano mwanamme unamkuta amevaa bukta haisitiri magoti au amekaa tumbo wazi mbele ya mke wa kaka yake. Au mwanamke kuvaa nguo za kubana au kutembea bila ya stara kichwani au vazi lolote lile analovaa ndani. Hayo yote ni makosa na hayafai ndani ya uislamu.

Tena la kusikitisha waume au wake wamekaa kimya wakidhani na wao ni sahihi au wanajua ovu bali wananyamaza. Na hili ni miongoni mwa sababu zinazopeleka kusikia kesi amemchukua mke wa kaka yake au mume wa dada yake. Ndio inachangia mume au mke anaona umbo la shemeji yake. Unadhani nini kitatokea?

Anasema Allah (subhanahu wataala) “Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.”(Suratu Nnur : 31).

Aya iko wazi hapo kuwa shemeji hajatajwa. Kwa nini waislamu tuige mila za mayahudi na manasara?
Pia imekatazwa kujipamba mbele ya shemeji. Kama tulivyosema yeye si maharimu yako hivyo hatakiwi akuone unapojipamba au ulivyojipamba. Ila hili ni msiba kwa wanawake wa sasa maana wanajipamba na wanaranda majiani waonekane na kila mwanamme.

2- Kukaa faragha au kutoka pamoja faragha. Shemeji si maharim yako. Hivyo haipaswi mukae faragha baina yenu. Ila jamii ilivyojisahau unamkuta mtu anarudi harusini usiku anaenda kuchukuliwa na shemeji yake. Wako peke yao wanarudi. Mtu na shemeji yake wanatoka peke yao bila ya maharim baina yao wanakwenda safari zao na kurudi. Haya nayo ni makosa. Na mume au mke ndio wa kwanza kusema mpeleke shemeji yako safari zake.

Kwa nini makosa? Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) anasema: “Mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho, basi asikae peke yake na mwanamke asiyekuwa maharimu yake pamoja naye, kwani watatu wao ni shetani” (Ahmad).

Mtume (Swalla Allahu alayhi wasallam) amesema: "Hawi faraagha mmoja wenu pamoja na mwanamke ila awepo Mahram wake" (Bukhari Na Muslim)

Hadithi zinaonesha moja kwa moja kuwa haya yenye kufanywa hayafai. Shemeji si maharim yako. Bora jamii ikuone tofauti kwa kufuata sheria za Allah (subhanahu wataala) kuliko kuwaridhisha wao na unamkera Allah (subhanahu wataala).

3-Miongoni mwa makosa mengine yanayofanywa ni kwa kupeana mikono wakati wa kusalimiana au waki zungumza, Amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allahu ‘alayhi wasallam): “Mmoja wenu kuchomwa [kudungwa] katika kichwa chake (na katika Riwaya: (cha mwanamme) kwa msumari au sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyekuwa halali kwake.” Imepokelewa na Atw-Twabaraaniy.

Mtu na shemeji yake wanapiga picha huku wameshikana mikono au kamkumbatia shemeji yake. Au mwanamke anapiga picha na shemeji yake wakati mwanamke amevaa vazi lisilo la kisheria. Wenyewe wanasema wanaishi kizungu. Ila tambua hayo yote ni makosa. Na haitakikani waislamu tuchukue mila za mayahudi na manaswara tujipambe nazo. Ni lazima tujiepushe nazo.Maana mambo haya yanafanywa na wasiokuwa waislamu na muislamu anafanya ili na yeye aonekane anaenda na wakati. Ila atambue yamekatazwa katika uislamu.

Na wala hatusemi mtu asizungumze na shemeji yake. Wazungumze wakae vizuri ila iwe chini ya muongozo uliowekwa na dini yetu. Na kufuata sheria za kiislamu ni kujenga heshima baina yenu na udugu uliokuwa bora. Utakaoepusha fitna na ugomvi baina ya ndugu na familia.

Na tambua ewe muislamu, uislamu haukuweka haya ila kwa maslahi. Kesi za shemeji zimezidi sana ndani ya jamii zetu. Tatizo sisi tuko mbali na maamrisho ya dini zetu na tumekumbatia mila za kikafiri. Nafsi ya mtu usiibebee dhamana.Kwani nafsi daima inaamrisha maovu. Allah (subhanahu wataala) anasema “Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu “ (Suratu Yuusuf : 53). Na huwezi kujua ni mbinu gani anazoweza kutumia sheytwan.

Ishi katika njia ya Allah ili upate furaha hapa duniani na kesho akhera.

Thursday 18 December 2014

NASAHA MUHIMU SANA KWA WATUMIAJI WA SIMU ZA MIKONONI,FACEBOOK,WHATSAPP NA MITANDAO MENGINE YA KIJAMII


Anasema Allah (subhanahu wataala) “Na tukambainishia zote njia mbili“(Suratul Balad :10). na akasema tena “Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.”(Suratul Insaan :3).

Aya mbili za juu zinaonesha ni vipi ambavyo Allah (subhanahu wataala) amempa uhuru wake mwanadamu. Allah (subhanahu wataala) amembainishia mwanadamu njia mbili. Na akamwambia njia hii ukiifuata basi utapata radhi zangu na ukiikataa njia hii ukafuata njia nyengine basi huko utapata ghadhabu zangu. Allah (subhanahu wataala) akamuacha mwanadamu achague mwenyewe ni wapi pakufuata. Na kumuacha huku si kwa lengo jengine ila ni kumpa mtihani. Anasema Allah (subhanahu wataala) “Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi.” (Suratul Mulk :2).

Wengi wa wanaadamu wameghafilika na uhuru walopewa. Na hakuna kinachowaghafilisha ila ni pumzi za dunia na starehe zake. Badala ya kufuata njia ya kheri amekuwa akiifuata njia ya shari na akafanya matamanio yake ndio mola wake. Anasema Allah (subhanahu wataala) “Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake”(Suratul Jaathiyah : 23).

Na mwanadamu huwa anajua kama amepewa uhuru huo. Kwani hata anapokumbushwa neno la Allah au kukatazwa usifanye hiki kibaya hujibu kaburi lako au langu? Pesa ninayoitoa yangu ya yako? Wewe inakuhusu nini? Yote hayo ni miongoni mwa majibu yake. Lakini kwa uwezo wa Allah tusichoke katika kuwakumbusha na kujikumbusha.

Sasa tuangalie uhuru wake mwanadamu na kipi ataenda kumjibu Allah (subhanahu wataala)?

1-Muislamu amepata simu kutoka njia yoyote ile iwe ya halali au ya haramu. Lengo la simu hiyo ni kwa ajili ya mawasiliano. Anajua mwenyewe yawe ya kheri au ya shari. Lakini hebu ajiulize yafuatayo : Mauti yakimfika na simu yake iko mkononi mwake au mfukoni mwake, Je Allah (subhanahu wataala) atakuwa radhi na yeye?

Ili Allah (subhanahu wataala) awe radhi nae maana yake kusikuwemo na lolote lile la haramu la kumkera Allah (subhanahu wataala).

Au Allah (subhanahu wataala) hatokuwa radhi nae kwa sababu ndani ya simu yake imejaa message za matusi,mapenzi na mazungumzo ya haramu? Au ndani ya simu yake imejaa namba za wanaume au wanawake ambao husema ni wapenzi wake wa haramu? Au ndani ya simu yake kuna video za ngono na nyimbo? Au yeye ameoa au ameolewa lakini hutumia simu yake kutoka nje ya ndoa? Au hutumia simu yake kuwadhulumu watu na kufanya mambo ya riba au kuiba?

Nini atamjibu mwanadamu huyu Allah (subhanahu wataala)? Je anajitengenezea njia gani kwa Allah? Hebu jiulize masuala haya sasa hivi ikiwa mtu atafikwa na mauti. Je simu yake inamridhisha Allah?

2-Muislamu anatumia facebook.Ikiwa facebook hiyo inatumika katika kheri na kwa ajili ya Allah pongezi kwako ewe ndugu yangu wa kiislamu. Je ikiwa facebook hiyo muislamu unaitumia katika dhambi nini utamjibu Allah (subhanahu wataala) baada ya kufikwa na mauti?

Malaika wa roho akija kukutoa roho huwa hakupi fursa ukafute picha za wanawake au wanaume ulizotumiana na wenzako. Hakupi fursa ukafute picha za uchi ulizopiga na kumtumia mwanamme au mwanamke. Hakupi fursa ukafute mazungumzo yako ya kimapenzi katika njia ya haramu. Hakupi fursa ukafute comment zako za matusi kwa watu. Hakupi fursa ukafute message zako za matusi ulizowatumia watu. Hakupi fursa ukafute yale uliyoyaweka katika kurasa yako na watu wanaona?

Je umeona uzito wake? Je kweli unalo jibu la kumjibu Allah (subhanahu wataala) ikiwa hali yako ni hiyo sasa? Malaika wa roho anarejesha roho kwa Allah inbox yako facebook imejaa picha na mazungumzo ya haramu. Facebook yako umeweka nyimbo na mambo mengine ya kuwafurahisha wanaadamu na kumkera mola wa walimwengu na ulimwengu. Anasema Allah (subhanahu wataala) “Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” (Suratu Nnuur:19).

3- Muislamu anatumia whatsapp. Ikiwa ni katika njia ya kheri basi Allah akuridhie. Je ikiwa ni kwa shari?
Muislamu husambaza nyimbo ndani ya whatsapp. Husambaza video za ngono na picha za ngono  iwe video hiyo kajirikodi yeye au picha hiyo kajipiga yeye au mwengine. Tena wengine husema wanaficha sura. Je unamficha mpaka Allah (subhanahu wataala) anaejua mpaka yaliyojificha ndani ya kifua chako?

Muislamu husambaza haramu yoyote ile na huku anacheka akiona anawafurahisha wenzake. Tena wako wanaosifiwa fulani kila siku hakosi jipya. Naam sifa za kidunia zimemlevya ila je anajua kuwa kila atakaengalia yale aliyotuma anapata dhambi? Je hajiulizi akifa leo watu wataangalia video zile au picha ile kwa miaka mingapi na ni wa ngapi wataangalia? Je anajua na yeye anapata dhambi kwani alichangia kusambaza uchafu? Allah (subhanhu wataala) anasema "Na hapana shaka wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Kiyama juu ya waliyo kuwa wakiyazua."(Suratul Ankabut:13).

  Wengine husambaza aibu za watu kwenye whatsapp,matusi na habari za uongo. Je malaika wa kutoa roho anakuja kuchukua amana ya roho. Nini atamjibu mola wa viumbe vyote?

Isituhadae dunia na vilivyomo ndani yake. Zisituhadae pumzi na kusahau akhera zetu. Tusifuate matamanio ya nafsi zetu. Tusije kujuta wakati huo wakati ambao majuto hayana tena faida. “Na watasema: Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa na akili, tusingelikuwa katika watu wa Motoni!." Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!.” Suratul Mulk : 10-11)

Turudini kwa Allah (subhanahu wataala) na tukae katika njia yake. Hata yule ambae kishayafanya basi akitubia kwa Allah tawba ya kweli basi Allah atamsamehe. Allah (subhanahu wataala) anasema “Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”.(Suratu Zumar : 53).
ALLAH TUJAALIE WALE WENYE KUAMBIWA MAZURI NA KUYAFANYIA KAZI NA KUKATAZWA MABAYA NA KUYAWACHA"Aaamin.

“Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.”(Suratul Baqara:281).

Makala Imeandaliwa na Raudhwah Islamic Group.

Friday 24 October 2014

UKUMBUSHO KWA WENYE KUFANYA MIJADALA NDANI YA MITANDAO YA KIJAMII NA KUISHIA MATUSI AU KUZUA NDANI YA DINI

Makala Imeandaliwa na Raudhwah Islamic Group

Kila sifa njema zinamstahikia Allah (subhanahu wa ta‘ala) Muumba wa kila kilichomo katika ulimwengu huu. Swala na salamu zimuendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allahu alaihi wa sallam).

Katika makala yangu ya leo nakusudia kupeleka nasaha zaidi kwangu binafsi pamoja na ndugu zangu wa kiislamu ambao hutumia mitandao ya kijamii kwa njia ya kujadiliana mambo mbali mbali ya kidini au ya kijamii.

Kumekuwa na maumivu makubwa ndani ya nafsi za waumini mbalimbali ambao huwa wanasoma maoni na mijadala ya dini ya waislamu ndani ya mitandao ya kijamii. Mijadala yenye hekima inafaa kwani inaleta funzo ndani ya jamii na kukosoana pale watu walipokosea. Ila mingi ya mijadala hiyo imekuwa haina heshima. Imekosa busara, na mwisho ni maneno machafu ambayo hata kuyaandika mfano wake siwezi. Leo nitajaribu kuyazungumza haya mambo kwa uchache ili tuweze kupeana tahadhari ili tusije kujuta siku ambayo mwanadamu hayatomfaa majuto yake. Miongoni mwa mambo yanayofanywa ni kama yafuatayo :

1-MATUSI YA NGUONI NA MANENO MACHAFU

Kwa hakika ukiwa unaangalia mijadala ndani ya facebook au whatsapp wengi wa watu huishia katika kutukanana na kutoleana maneno machafu. Ikiwa muislamu mwenzako hakubaliani na msimamo wako basi usimtukane wala usimwite majina mabaya au kumwambia maneno yasiyofaa. Tumia hekima katika kumfanya yule mtu aweze kukufahamu na aweze kukuelewa kile unachokikusudia. Lau angekuwa Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam),masahaba zake na wema wengine waliopita kazi yao kutukanana tu katika kufikisha daawa kweli uislamu ungekuwa na hali gani?

Daawa yao na mijadala yao ilikuwa ni daawa iliyojengwa na misingi ya Allah (subhanahu wataala) iliyotajwa ndani ya Quraan “Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka”(16:125)

Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) anaambiwa hata akijadiliana na wasiokuwa waislamu basi ajadiliane nao kwa namna iliyobora. Vipi baina ya muislamu kwa muislamu mwenzake? Vipi mazungumzo ya muislamu na muislamu mwenzake? Unadhani kuandika matusi na maneno yasiyofaa ndio utakuwa mtetezi wa uislamu? Hapana bali utakuwa ndio mpingaji wa aya za Quraan. Hebu tuangalie ndani ya Suratul Hujurati Allah ndani ya aya ya 11 Allah (subhanahu wataala) anasema “Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini.” Je haya yote waislamu tunayasahau?

Kumtukana muislamu mwenzako na asiyekuwa muislamu ni makosa ndani ya dini yetu. Tutumie lugha nzuri na laini baina yetu na baina ya wasiokuwa waislamu. Na yule ambae atakutukana basi wewe usirejeshe kwa tusi fahamu kuwa bado hajaijua haki siku akiiijua hatofanya hivyo.

Tuwe wapole na wenye kuheshimiana daima baina yetu.

2-KUZUSHWA KWA HADITHI ZA UONGO

Wakati watu wanapojadiliana wako watu huvuka mipaka na kuzusha yale yasiyokuwemo ndani ya dini. Wako wanaotunga hadithi na wako wengine wanaotoa fatwa kwa mambo wasiyokuwa na elimu nayo.

Ndugu zangu wa kiislamu tumuogopeni Allah (subhanahu wataala) tusitunge au tusiseme jambo ambalo halimo ndani ya Quraan wala sunna. Kama jambo hulijui ni bora kukaa kimya kuliko kuzua. Je unajua ni yapi yanayomsibu mwenye kuzua katika dini? Kutoka kwa Bibi Aisha(Radhiya Allahu anha) kuwa Mtume (Swalla Allahu alayhi wa aalihi wasallam) amesema : “Atakayezua akatia katika Dini yetu hii ambacho hakiko atarejeshewa mwenyewe.” (Al Bukhaariy na Muslim).

3-KUJITUKUZA KWA MTU KWA DHEHEBU LAKE AU ELIMU YAKE

Wako watu huwa wanajigamba na kujisifu kutokana na misimamo yake. Na huwa anaona ni rahisi sana kuwaambia waislamu wengine kuwa ni watu wa motoni na yeye na wenye kufuata madhehebu au misiamamo aliyokuwa nayo yeye ndio watu wa peponi na wako sahihi. Ni nani aliyekupa darja ya kuwaweka watu peponi na motoni? Ni nani aliyekwambia wengine uwadharau. Huo sio uislamu.

Tukhitalifiane lakini tusitoane kwenye uislamu wala tusiingizane motoni. Kwani hiyo ni kazi yake Allah (subhanahu wataala) peke yake. Bali sisi tukae kwa upendo nah uruma baina yetu. Allah (subhanahu wataala) anasema “Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.”(53:32).

Wako wengine wao hujiona ndio wenye elim una ndio wana haki ya kusema kila kit una wasemalo wao ndio sahihi ya wengine si sahihi. Huku ni kukosa kwa elim una adabu zake. Na inampasa muislamu ajiepushe na tabia hizo. Kwani kujionesha na kibri kuna makatazo makubwa ndani ya uislamu. Imepokelewa kutoka kwa Abdullah bin Masud (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) amesema:"Hatoingia Peponi ambaye moyoni mwake mna chembe ya kiburi". Mtu mmoja akauliza: “Mtu hupenda nguo yake iwe nzuri na viatu vyake viwe vizuri (itakuwaje?)” Akasema: "Hakika Allaah ni Mzuri Anapenda Uzuri. Kiburi ni kukataa haki na kudharau watu)"Muslim

Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) :“Ninachokuogopeeni sana ni Shirki ndogo.)) Maswahaba wakauliza: "Ni nini hii Shirki ndogo, ewe Mtume wa Allah?" Mtume (Swalla Allahu alayhi waaalihi wasallam) akasema: Riya (kujionyesha).” [Imepokewa na Imaam Ahmad]

Nasaha zangu kwa waislamu tutumieni mitandao ya kijamii kwa uzuri. Daima tujue kuwa kila tunalolifanya linaandikwa na tutakuja kuyakuta katika kitabu chetu. Tuitumie mitandao hii kwa kujua kuwa Allah (subhanahu wataala) anatuona. Ikiwa binaadamu mwenzako unamuonea haya akuone ukiwa katika jambo ovu je huoni haya jicho la Allah likiwa linakuona unamuasi yeye na unafanya kinyume na alivyoamrisha?

Tutubieni kwa Allah (subhanahu wataala) toba ya kweli na tuache kabisa yale tuliyokuwa tunayafanya. Allah (subhanahu wataala) anasema “Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.”(50:19). Na anasema tena Allah (subhanahu wataala) “Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma.”(36:65). Tukumbuke aya ya Allah (subhanahu wataala) isemayo ““Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.”(2:281).

Thursday 23 October 2014

JINSI YA KUITUNZA NDOA YAKO

Makala kutoka Raudhwah Islamic Group

BISMILLAHI RRAHMANI RRAHIM

Namshukuru Allah kwa kunipa nafasi hii ya kuandika makala adhimu kama hii ambayo endapo itafanyiwa kazi na Allah سبحانه وتعالىakaitilia Tawfiq basi itakua ni sababu ya kuleta manufaa makubwa katika jamii. Kisha swala na salam zimuendee kipenzi chetu Mtume Muhammad (sawﷺ).

Ama baada ya utangulizi huo sasa nitaingia rasmi katika uwanja mpana wa ndoa. Na leo nimependa kuzielekeza nasaha zangu zaidi kwa upande wa kina dada Ni jinsi gani watazilinda ndoa zao.

Kama tunavyofahamu ya kuwa ndoa ni mafungamano ya hiari baina ya mke na mume kuishi kwa pamoja kwa mapenzi na huruma mpaka mwisho wa maisha yao. Hivyo kwa kutambua hili inabidi kila mmoja wao awe ni mwenye pupa katika kuyafanya mambo ambayo yatakayozidisha mapenzi ya mwenza wake ili lipate kupatikana lengo kuu la ndoa ambalo ni utulivu wa nafsi.

Leo nimependa kuwabainishia mambo ambayo endapo mke atamfanyia mumewe basi yatazidisha mapenzi makubwa kwa mumewe kwani wengi wetu tunashindwa kuyafahamu ima kwa ufinyu wa fikra zetu au kwa sababu ni wapya katika ndoa.
Yafuatayo ndio mambo yakumfurahisha mumeo ili kuiimarisha ndoa yako:

1-KUWA MTIIFU KWAKE KATIKA MEMA ANAYOKUAMRISHA.

Tukizungumzia suala la utiifu ninamaanisha kuyatekeleza yale anayoyataka uyafanye katika yale yanayoridhiwa na Allah (subhanahu wataala). Kila binaadamu huwa ana mambo anayoyapenda afanyiwe na anayoyachukia yani hapendi afanyiwe. Na hali hii inatofautiana kutokana na mtu mmoja na mwengine. Kwa kua kuna mambo ambayo wengine kwao ni kawaida lakini kwa wengine huwa ni kero..Mfano Kumwita mumeo majina mazuri ya mapenzi kama mpenzi, laazizi, honey wapo wanaume ambao wanapenda na wanajihisi fahari kwa kuitwa majina haya na wake zao ima wakiwa peke yao au mbele za watu. Lakini wengine huwa hawapendi au wanapenda waitwe majina mazuri wakiwa faragha na wake zao au hupendelea kuitwa majina yao halisi. Katika hali hii inabidi mke uende na namna mumeo anavyopenda na sio kumwita kwa namna upendavyo wewe. Nadhani nitakua nimefahamika katika hili.

Na Kumtii mume ni katika ibada takatifu sana ambazo humpeleka mwanamke peponi atakapoifanya na kumuingiza motoni atakapoenda kinyume nayo. Amesema Mtume(ﷺ) “Atakapo swali mwanamke swala zake tano(za faradhi), akafunga mwezi wake (wa ramadhani), akajihifadhi utupu wake (kwa stara inayotakikana na hakutoka nje ya ndoa yake), na akamtii mumewe ataambiwa siku ya kiama INGIA PEPONI KWA MLANGO UUPENDAO” Imepokelewa na Imam Ahmad.

Pia suala la kumtii mume ni katika ishara za imani. Kwani Allah Subhanahu wataala amesema katika Qur'an tukufu :((Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi...))(4:59) .Na katika wenye madaraka juu yetu sisi wanawake ni waume zetu ambao wamekubali kuchukua dhima kutoka kwa wazazi wetu. Hivyo ili kuipata imani ya kisawa sawa inabidi tuwe watiifu kwa Allah, Mtume na Waume zetu bila ya kuwasahau wazazi wetu kwani nao bado wanahaki na sisi. Allah atuwafikishe katika hili.

2-Ridhika na Alichonacho

Katika mambo ambayo huongeza mapenzi mno katika ndoa ni wanandoa kutosheka. Namaanisha kwamba kila mmoja awe ameridhika na hali yoyote atakayomkuta nayo mwenzake. Na hawi na sifa hii ila yule mwenye mapenzi ya dhati kwa mwenzake na pia mwenye imani katika kifua chake kwani hakika muumini siku zote hutosheka na alichonacho na kuridhia kwamba ni qadar ya Allah (subhanahu wataala) aliyomkadiria. Amesema Mtume (ﷺ) : (( Ridhia katika kile alichokugawia Allah utakua ni tajiri zaidi kuliko watu)) Attirmidhiy.

Na pia katika hadithi nyengine amesema Mtume (ﷺ) “Hakika amefaulu aliesilimu na akaruzukiwa kinachomtosheleza na akakinaishwa na Allah kwa kile alichomruzuku”. Muslim.
Hadithi hizi mbili zinatufundisha tuwe wenye kukinai na kile tulichoruzukiwa kwani ni sababu ya kufaulu hapa duniani mpaka kesho akhera.

3-MTUNZIE SIRI ZAKE

Hakika katika mambo yanayochukiza mbele ya Allah (subhanahu wataala) na yatakayomsababishia mtu kupata adhabu kali ni mke au mume kutoa siri za mwenzake kwa nia mbaya yaani kumfedhehesha. Kwani amesema Mtume (ﷺ) katika kuelezea hili: ((Hakika katika watu wenye nafasi mbaya siku ya Qiyaamah ni mwanaume anaemuendea mkewe au mke anaeendewa na mumewe (wakafanya tendo la ndoa) halafu akaeneza siri ile)). Muslim. Hadithi hii imemkemea kila mwanaume na mwanamke mwenye kueneza siri za mwenzake.

Hivyo ni wajibu wetu kuwa makini na hili kwani tutakapojiepusha nalo tutakuwa miongoni mwa wanawake wema.

4-MUAMINI MUMEO

Uaminifu baina ya wanandoa ni jambo muhimu sana linalopelekea ndoa kuwa madhubuti ama kinyume na hapo ndoa hulega lega na kupelekea kuvunjika. Katika suala la uaminifu kila mmoja anatakiwa kuwa ni muaminifu kwa mwenzake sawa sawa wapo karibu au mbali mbali.

Muamini mumeo na wala usimtilie mashaka kwani kumtilia mashaka kutakuondolea mapenzi katika moyo yako. Na pia usichukue hatua yoyote kwa jambo la kuambiwa haswa litakapotoka kwa mtu ambae anajulikana kwa tabia zake kuwa ni mfitinishaji na ni mchochezi baina ya ya watu. Kwani hata Allah Subhanahu Wataala ametuambia ndani ya Qur'an : ((Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.)) 49: 6

Hivyo utakaposikia jambo lolote baya kuhusu mumeo ni bora kulihakikisha mwenyewe kwa macho au masikio yako ili usije ukaharibu ndoa yako kwa sababu zisizo na msingi.

5-JIPENDEZESHE KW AJILI YAKE

Tambua ewe dada wa kiislamu kwamba kujipamba kwa ajili ya mume wako ni ibada na utalipwa kupitia ibada hio. Utakapopenda kujipendezesha kwa ajili ya mumeo kwa namna mbali mbali zilizo za kheri (zinazoruhusiwa na sheria) basi mumeo hatakuchoka na kinyume chake atatamani kila anapopata fursa akimbilie ndani kwake kwani wewe mkewe ni sababu ya tulizo la macho yake na moyo wake.

Kinyume na hapo mke ukiwa hujipambi kwa ajili ya mumeo kwanza unapata madhambi kwa sababu wewe ndio unakua chanzo cha yeye kutafuta tulizo la jicho na moyo wake katika vilivyo vya haramu. Pili wewe kama utakua unajipamba nje ya nyumba yako basi nawe utakua unapata madhambi kwani Allah(subhanahu wataala) ametukataza kuyabainisha mapambo yetu ila kwa wale wasioruhusiwa kutuoa yani baba, kaka, mjomba, babu, baba mkubwa au mdogo na watu wanaokuhusu kwa damu au ulionyonya nao.

Allah(subhanahu wataala) anatuambia: ((Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.))24:31

Aya hii nadhani haihitaji ufafanuzi kwani yenyewe ilivyo imejitosheleza. Na ametukuka Allah kwani hatuamrishi ila lililo na kheri nasi na hatukatazi ila lililo na madhara nasi duniani mpaka kesho akhera.

Saturday 18 October 2014

SIMU ZA MIKONONI NA NDOA ZETU

Makala hii Imeandaliwa na Raudhwah Islamic Group.

Kila sifa njema zinamstahikia Allah (subhanahu wa ta‘ala) Muumba wa kila kilichomo katika ulimwengu huu. Swala na salamu zimuendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allahu alaihi wa sallam).

Kwa hakika katika elimu aliyowajaalia Allah (subhanahu wataala) waja wake ni uvumbuzi wa mambo mbalimbali. Katika yaliyovumbuliwa mengine huwa na faida na mengine huwa na hasara. Simu ya mkononi ni miongoni mwa kifaa kilichovumbuliwa. Simu ina faida zake ikiwemo kurahisisha mawasiliwano baina ya mtu na mtu mwengine,kuweka ukaribu kwa familia au marafiki. Lakini kwa hakika kwa sasa simu ina madhara makubwa sana kwetu sisi. Na ni wachache sana ambao wamesalimika na fitna hizi au madhara yake.

Leo katika makala hii nakusuduia kuzungumzia jinsi simu za mikononi zinavyoharibu ndoa zetu na hata kupelekea kuvunjika kwa ndoa hizo. Ziko ndoa nyingi sana zimekwisha kwa wanawake kupewa talaka au kwa kuomba talaka na sababu kubwa simu za mikononi. Namuomba Allah ajaalie tawfiq iwe ni sababu kwa kila atakaesoma makala hii ya kujirekebisha pale alipokosea.

1-MAZUNGUMZO YA KIMAPENZI BAINA YA MWANANDOA NA MTU AMBAE SIO MWANANDOA MWENZAKE

Ni simu ngapi ndani yake zimekutwa na ujumbe wa kimapenzi. Ujumbe ambao mtu hajatumiwa na mke wake au mume wake. Tena huwa ni ujumbe wa mapenzi unaoshiria kuwa mke au mume ni mwenye kutoka nje ya ndoa yake. Linapotokea jambo hilo kwa wanandoa wako wengine hujifanya mafundi wa kusema uongo na wengine huishia kutoa maneno na kukosa jibu. Au mwanamme kujifanya yeye ndio bwana hatakiwi kuhojiwa. Na hata wengine huishia kupiga wake zao kwa sababu tu ya kushika simu yake.

Kwa nini mtu ukose uaminifu kwa mwanandoa mwenzako? Kwa nini utumiwe ujumbe wa kimapenzi na mtu asiyekuwa mume wako au mke wako? Hivi unadhani hesabu yako hutaikuta kwa Allah? Kwa nini simu imekuwa inawekwa password ambayo haambiwi mke ikiwa na mume au haambiwi mume ikiwa ni mke? Tunakwenda wapi enyi umma wa kiislamu? Kwa nini tunazifisidi ndoa zetu kwa kufuata matamanio ya nafsi zetu?

Napenda kutoa nasaha kwa wanandoa unapokuta ujumbe ambao unaashiria machafu kwa mume wako au mke wako basi usikimbilie kutoa maneno au kufanya yasiyostahiki. Kwanza uliza kwa hekima na uwe na subra yawezekana ni fitna tu imeundwa ili kukuharibieni ndoa zenu. Na haya yapo na tayari yameshavunja ndoa za watu kumbe ni jambo lililopangwa na kuzuliwa. Kwani Allah (subhanahu wataala) anasema “Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.”(49:6). Ndio chunguza kwanza ili baadae usije kujuta kwa kumuingiza mwenzako kwenye makosa yasiyokuwa yake.

Na ewe uliyeoa au kuolewa acha tabia za kutoka nje ya ndoa yako. Umeaminiwa basi na wewe jiaminishe. Kwani hakika ni alama ya unafik yule anaeaminiwa akavunja uaminifu wake. Tambua kuwa Allah (subhanahu wataala) anakuona na tambua hakuna la siri kwake na ipo siku siri hiyo itatoka tena itakuwa ni siku ya majuto makubwa na fedheha. Na mwisho wake kuingia katika moto. Allah atuhifadhi. Allah (subhanahu wataala) anasema “Siku zitakapo dhihirishwa siri.”(86:9).

2-KUKUTWA NA PICHA ZISIZOKUWA NA HESHIMA NDANI YA SIMU

Siku hizi kuna whatsapp na facebook hizi nazo zina mchango mkubwa sana kuharibu ndoa zetu. Mwanamme anakuwa na picha za wanawake wakiwa hawana mavazi au mwanamke nae kukutwa na picha za wanaume. Je unadhani ni lipi ambalo mume wako au mke wako ataweza kulifahamu akikutana na hali hizo?

Picha kama hizi zinapatikana kwa aina mbili kuu kwanza ni picha zinazoezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu ambao hawana khofu juu ya Allah na ni wenye kumuasi Allah (subhanahu wataala). Na pili huwa ni picha ambazo mwanamke au mwanamme ameziomba kwa watu wao ambao hufanya mambo ya haramu.

Umeoa au umeolewa kwa lengo upate utulivu wa nafsi. Na ukapewa uhuru uoe katika uwapendao na uolewe na yule umpendae. Sasa hili suala la kutafuta picha zisizokuwa na maana ten aza haramu zinatoka wapi?

Tena wanandoa wengine wanakutwa na picha hizo wakiwa na wanaume zao au wanawake zao ambao wanafanya nao maasi hali ya kuwa na wao wameolewa au wameoa? Ni wanawake wangapi au wanaume wangapi tayari wameshakutwa na kesi ya kukutwa na picha za wanaume au wanawake ambao sio jamaa zake ziwe za heshima au sio za heshima? Lazima mke au mume ataumia kwa sababu ya wivu. Haya yote yanasababishwa na simu zetu za mikononi. Tujiepusheni na tabia hii ili kuzilinda ndoa zetu.

3-KUJIFICHA NA SIMU WAKATI WA MAZUNGUMZO

Wengi wa wanandoa wenye kutoka nje ya ndoa zao huwa wanaogopa kuzungumza na simu mbele ya wake zao. Na ikiwa anazungumza huwa anajifanya huyo mtu hamjui kabisa au huwa anababika katika mazungumzo. Na wako wengine hasa wanaume wanapoingia kwenye nyumba zao huzima simu sababu kubwa husema hataki kukerwa ila ni wachache wenye ukweli. Wengi wao hukimbia kutumiwa ujumbe na wanawake au kupigiwa simu na wanawake wa haramu. Kwa nini simu ikiwa kwako tu ndio inazimwa? Basi itoe sauti iweke pembeni.

Itunze ndoa yako. Usiweke mazingira ya mwenzako kukutilia shaka na itakuja kupelekea kuondosha uaminifu kwenye ndoa yenu.

Kwa hakika mada hii ni refu na ina mifano mingi sana. Naomba niishie hapa na nitoe nasaha zifuatazo : Simu zetu zisituhadae hadi tukawa tayari kuvunja ndoa zetu na zikatupeleka pabaya siku ya Qiyama. Tumuogopeni Allah (subhanahu wataala). Hebu kaa na utafakari ni pesa ngapi umehonga kwa wanawake au umetumia kwa ajili ya wanawake wakati mke wako wa halali unae ndani nae ana shida zake nyingi sana? Tambua unatumia neema za Allah na utakuja kuulizwa juu ya neema hizo. Ewe mwanamke itunze ndoa yako na usikubali kuipoteza ndoa yako kwa kukosa uaminifu. Dunia ni hadaa na hesabu zetu zote tutazikuta kwa Allah. Tukumbuke aya ya Allah (subhanahu wataala) isemayo ““Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.”(2:281).

Sunday 31 August 2014

Muenzi Mke Wako

Imeandikwa na Shaykh 'Abdullaah 'Adhamiy

Imefasiriwa na Iliyaasa

Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi.

Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.

Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.  

Kielezo bora kabisa ambacho mimi binafsi nishawahi kusoma kinafafanua ukaribu wawanandoa juu ya wao kwa wao na kielezo hicho kipo katika aya ya Qur-aan ambayo inasema:

((Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao)) [Al-Baqarah 2:187].

Na Kweli, wanandoa ni kama vazi juu ya wao kwa wao kwa sababu wanapeana ulinzi, liwazo, kinga (stara), msaada (tegemeo), na mapambo ambayo vazi linampa mtu. Hebu jaribu kufikiri msafara wakati wa siku za baridi kwenda sehemu kama vile Alaska bila ya kuwa na nguo! Wanandoa wetu wanatupa kiwango kile kile cha faraja (liwazo), ulinzi, na msaada  katika msafara wa maisha yetu katika dunia hii kama vile nguo itakavyofanya katika msafara wa Alaska.

Mahusiano baina ya wanandoa ni ya kustaajabisha kabisa katika mahusiano yote ya kibinaadamu: Idadi ya mapenzi na mahaba, undani na ukaribu, huruma na imani, amani na utulivu ambao unajaza nyoyo za wanandoa ni jambo lisiloelezeka kwa wepesi. Ufafanuzi pekee wa mantiki ambao unaweza kuelezeka juu ya haya mastaajabu makubwa katika hisia zote za kibinaadamu ni kwamba: Ni kitendo cha Allah Subhanahu wa Ta'ala, ((Na Allaah Amekuumbieni wake [na wenza katika jinsi yenu])) [An-Nahl 16:72]

Mola wetu tu Allaah Subhanahu wa Ta'ala katika katika Utawala Wake usio na upeo wa huruma Yake  isiyo na mipaka  na Hekima Yake adhimu Anaweza kujenga na kuzididimiza katika akili hizi hisia za kustaajabisha na za kubarikiwa katika nyoyo za wanandoa. Kwa kweli Allah Subhanahu wa Ta'aala Anawakumbusha wale ambao wanatafuta ishara Zake katika ulimwengu huu kwamba hisia hizi katika moyo wa wanandoa ni katika ishara Zake ambazo zinatakiwa zimuongoze mwanaadamu katika kuwepo Kwake kama Alivyosema katika Qur-aan, (Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri." [Ar-Ruum 30:21]

Lakini Allaah Subhanahu Wa Ta’aala Anajua kwamba moyo wa binaadamu sio kitu ambacho kiko tuli, wakati mwengine huwa dhaifu na wakati mwengine huwa na nguvu. Hisia zinaweza kubadilika na hubadilika pindi wakati unavyosogea. Mapenzi yanaweza kufifia na kupayuka mbalini. Mshikamano wa ndoa unaweza kuwa dhaifu kama haujahudumiwa vizuri. Furaha katika ndoa haiwezi kudharauliwa; furaha ya kuendelea inahitaji utowaji wa daima kutoka pande zote. Ili mti wa mapenzi ya ndoa ubaki hai na kuendelea kuishi, udongo lazima udumishwe, uhifadhiwe, umwagiwe maji na ulelewe.

Kumbuka kwamba Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipata nafasi ya kwenda kwenye majangwa na kushindana mbio na mke wake Bibi 'Aaishah. Bibi 'Aaishah alimshinda Mtume lakini baadae aliponenepa, Mtume alimshinda Bibi 'Aaishah. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimchukua mkewe kwenda kuwatazama vijana wa Ki-Ethiopia wakicheza michezo ya utamaduni wao. Maonyesho ya hisia yanahitajika kuweza kuufanya mshikamano wa ndoa usifanye kutu na kuoza. Kumbuka kwamba utapata thawabu kutoka kwa Allah (Subhanahu wa Ta'aala) kwa hisia zozote unazomuonyesha mkeo kamaMtume   (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyosema: ((Mmoja wenu atapata thawabu kwa chochote ambacho atafanya ili kutafuta radhi za Allaah hata kwa tonge analomlisha mkewe))

Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kuweka chakula kwenye mdomo wa mkeo, kumfungulia mlango wa gari, na hali kadhalika. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasogeza goti lake kwa mkewe amkanyage kuweza kumpanda ngamia.

Jaribu kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja. Kuuimarisha uhusiano kati yenu na Allaah (Subhanahu wa Ta'aala) ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubuti. Kuwa na amani kati yenu na Allah (Subhanahu wa Ta'ala)  daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi.

Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa habari nzuri (aliwabashiria) wanandoa wanaoamka usiku kuswali pamoja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anamsisitiza mwanandoa anayeamka mwanzo amuamshe mwenzake, japo kummwagia maji katika uso wake. 

Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:((Wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao))

Mwishowe, ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu wanandoa wenziwe mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo tu. Lazima upende anachokipenda pia. amilia yake, anaowapenda yeye uwapende pia. Usiwe kama mwenzangu mmoja ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia wazi mkewe “Mimi siwapendi wazazi wako”. Bila ya kusita mkewealimtazama machoni kwa hasira na kusema, “Na wako pia siwapendi”.

Mapenzi yasiishe na pia tunaamini kuna maisha baada ya mauti ambapo wale ambao walifanya wema katika dunia hii wataungana na wanandoa wenzio ((Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo)) [Az-Zukhruf 43:70] Pia wataungana na watoto wao.

Na mfano bora katika mintarafu hii itakuwa ni Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye mapenzi yake kwa Bibi Khadiyjah, mkewe aliyeishi naye kwa miaka 25 yalisogea mpaka kwa wale aliowapenda Khadiyjah; mapenzi yake haya yaliendelea hata baada ya kufa Bibi Khadiyjah. Ilikuwa miaka mingi baada ya kifo cha Bibi Khadiyjah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumsahau na kila panapochinjwa mbuzi katika nyumba yake basi hutuma kifurushi kwa familia ya Bibi Khadiyjah na marafiki zake na kila akihisi kuwa mgeni  anayegonga mlango ni Dada ya Khadiyjah aitwaye Hala, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba huku akisema, "Ee Allaah Jaalia awe ni  Hala."

Tuesday 19 August 2014

Zingatia haya yatakusaidia

Kuachana na swala inamaanisha kwamba utakosa raha ya nafsi katika dunia hii..amesema Mwenyezi Mungu: Na anayepingana na utajo wangu hakika atapata maisha ya dhiki

Hao ni wenye matumaini wale wanaoshibisha roho yako tamaa na kukusukuma kufanya kazi, wanakuliwaza kwa hekima kutokana na mateso yako na wanayapoza, na wanairutubisha furaha yako na wanatia nguvu ndoto yako na wanaiamsha..hao wafanye marafiki

Kama unataka kugeuza nafsi yako na kuipaisha kwa kiwango bora, huna budi utambue kwamba hatua ya kwanza ya mageuzi inatoka ndani yako... mageuzi yanaanza kwa nia ya mageuzi

Juu yenu kutubu.. kwani ina faida kwenu kuliko faida ya upanga
-alfudhail bin 'ayyaadh

Kuwa mtu mwema kwa unaowapita wakati unapanda kileleni.. kwani utakutana nao wakati unateremka! hakuna mmoja anayebaki kileleni maisha yote
  -steven cofey

Mtume Muhammad SAW alikusanya baina ya taqwa na tabia njema, kwani kumcha Mwenyezi Mungu ni baina ya mja na Mola wake, na tabia njema ni baina yake na viumbe
   -ibn alqayyim

(watapambwa kwa bangili za dhahabu) peponi; mapambo kwa wote, wanaume na wanawake..ni peponi.. huko kuna vinavyotamanisha nafsi na kuburudisha macho na kayafurahisha

Imepokewa na Jarir bin Abdallah amesema: Amesema Mtume SAW:

Amesema Mtume Muhammad SAW: hakika salaam (amani) ni jina miongoni mwa majina ya Allah SW lililowekwa kwenye ardhi, basi enezeni salamu baina yenu>>

Amiliana kwa wema kwa anayestahiki na asiyestahiki, kwani wewe unatafuta nyumba ya peponi si nyumba kwenye moyo wa kila mtu

Izoeshe nafsi yako kwenye mambo matatu:
- ukifanya jambo kumbuka Mola anakuona,
-na ukiongea ujue Mola amekusikia,
-na ukinyamaza elewa kwamba Mola anajua unachofikiri
  -hatim al asam

Wanadamu ni watu wa ajabu.. wanatenda kwa ajili ya dunia, huku wakiruzukiwa bila  amali..na wala hawafanyi kwa ajili ya akhera, ambapo hawataruzukiwa ila kwa amali

Kuchora tabasamu ni jambo jepesi ambalo unalifanya na kwa ujira mkubwa

Kila kitu inawezekana kukinunua ila nia nzuri, hiyo chimbuko lake linatoka kwenye kisima cha kichawi ndani ya nyoyo safi

Kila starehe isiyokuwa kwa ajili ya Allah, itabadilika na kuwa majuto kwa aliyeifanya siku ambayo ukubwa wake ni miaka elfu hamsini! mwenye akili ni yule anayestarehe mara mbili.. hapa duniani kwa twaa ya Mwenyezi Mungu, kisha peponi

Jiondoshee hisia za mateso, na mateso yenyewe yataondoka
-marcus aurelios

Mvivu hahisi thamani ya raha, kinyume na mchapa kazi ambaye anifurahia baada kufanya juhudi, akitaka kurudisha nguvu zake

Ewe Mola waponye wagonjwa waislamu, na walishe wenye njaa, na warudishe waliopotea, na waachie huru wafungwa wao, na warehemu maiti wao, na wape usalama na amani popote walipo katika ardhi hii ewe Mola wa viumbe vyote

       

Thursday 10 July 2014

Hebu jiulize masuala haya.....


HEBU jiulize masuala haya na lifikirie katika akili yako kila suala jibu utapata mwenyewe 
Mimi ni nani katika hii dunia?

Nimeishi miaka mingapi hadi sasa?

Nimebakiza miaka mingapi ya kuishi?

Nimefanya mangapi kwa ajili ya akhera yangu?

Maovu mangapi nimetenda kwa kuteleza au kwa makusudi?

Lini nilitoa chozi kutubu mabaya yangu? 

Lini nilikaa faragha na kumshukuru M/Mungu kwa wema anaonitendea? 

Hivi Mungu akichukua roho yangu wakati huu, nimebeba kazi (amali) ngapi za kheri zitakazo nisaidia?.

Nitakumbukwa kwa wema gani niliowatendea wanadamu na viumbe wengine?

ZINDUKA NDUGU YANGU.DUNIA ISITUHADAE TUKAMSAHAU MUNGU. Wakumbushe na wengine.

Hakika Halali Iko Wazi Na Haramu Iko Wazi


Kutoka kwa- Abu Abdullah An-Nu’uman Ibn Bashiyr -(RA) -ambaye alisema: Nilimsikia Mtume Mohammad (SAW) akisema:

Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui.-- Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka- anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchungaji anayechunga (wanyama) pembezoni mwa mpaka, mara- huingia ndani (ya shamba la mtu).- Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo Yake. Na hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama kikitangamaa, kiwiliwili chote hutangamaa, na kikharibika kiwiliwili chote huharibika. Basi jua (kipande hicho cha nyama) ni moyo.

Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim

Wasia wa Luqman Kwa Mwanae (Na kwetu sisi sote)


Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh;

Katika makala hii fupi, utapata ingawa kwa ufupi wasia alioutowa luqman kwa mwanae. Kwa hikma ya kisa hiki cha mja huyu mwema ndani ya Qur’an ni kwa malengo yetu sote na pili umuhimu wetu kuwa nasihi watoto wetu katika ibada.

Katika nasaha alizompatia mwanawe ni kuwatendea wema wazazi, kutokua na kibri, kusimamisha Swalah, kuamrisha mema na kukataza maovu, kusubiri, kutonyanyua sauti na kadhalika kama Alivyotupa maelezo hayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

‘Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Allaah Atakileta. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye khabari za yote’. -

‘Ewe mwanangu! Shika Swalah, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa’

‘Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Allaah Hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha‘ [Luqmaan:16-18]
Mahmoud Al-Asmi at 18:30

Kuwadanganya wanawake


Mmoja wa wenye hikma alisema: 
Jihadhari na kuwadanganya wanawake, kwani wana uhodari wa kujua ukweli, na uwezo mkubwa wa kujifanya hawajajua...!

"Mwenye kupoteza penzi la mwanamke muaminifu, amepoteza maisha yake yote"

- Je unajua kwamba......

1- mwanamke akiwasiliana nawe sana inamaanisha hataki kuongea na mwengine..?

2- mwanamke atapata mwanamme bora kuliko wewe kwasababu amejifunza kuchagua kwa jeraha lake.....

3- mwanamke aliyedhulumiwa, mwanamme atamrudia wakati akiwa ameshachelewa... (too late..!!)

4- mwanamke anamiliki hisia ya sita zaidi ya mwanamme kumjua akibadilika au akimkhuni.......!

5- mwanamke anasubiri na kuvumilia sana kuliko mwanamume.. na akimuacha mwanamme basi ni baada ya kujaribu kumuomba msamaha mara elfu..

6- mara nyingi mwanamke akiungulika anapendelea kunyamaza.....

7- mwanamke anaporeact na kukulaumu hii inamaanisha mapenzi yake mingi kwako...

8- mwanamke anapokua amekerwa na mwanamme ananyamaza kwa kutaraji kuwa atabadilika na sio kwa kutojua....

9- mwanamke akizungumziwa na mwanamme kuhusu mwanamke mwengine, huficha kilio chake nyuma ya tabasamu lake......

Mtume Mohammed (saw) kamfananisha mwanamke na chupa ya kiyoo tuibebe pole pole isituponyoke ikavunjika

Na maana yake tuishi nao kwa wema sana.

April fool na Uislam


Sitaki kuzungumzia asili ya April Fool day ili kufupisha mada yangu. Kila mmoja akae atafute asili ya April fool ni ipi basi muislamu wa kweli hakika hatokuwa pamoja na waongo na atajiepusha na kusema UONGO.

Ninachotaka kukizungumzia hapa ni hichi kitendo cha waislamu kusema Uongo kila ikifika tarehe mosi April. Uongo ni haramu haramu tena ni haramu. Na kuna makatazo makubwa ndani ya uislamu kuhusu Uongo. Leo muislamu anasema uongo kumwambia mwenzake je hakai akafikiria kuwa anaweza kumsababishia muislamu mwenzake kupata madhara? 

Leo unamwambia mtu aende sehemu kuna ajali au lolote je unajua mwenzako yuko katika hali gani wakati unampa habari hiyo? Halafu muislamu anacheka na kujidai kuwa amempata siku ya wajinga.

Mtume(swalla Allahu alayhi wasallam)anasema"Uongo ni haramu japokuwa ni maskhara"Katika jambo la kusema uongo waislamu tumekatazwa na tumetakiwa tuwe nalo mbali kabisa na kuna maonyo makali kutoka kwa Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam). Kutoka kwa Muaawiyah bin Haydah Amesema: " Nimemsikia Mtume Swalla Allaahu alayhi wasallam akisema:"Ole wake kwa anayehadithia jambo la uongo ili watu wacheke. Basi ole wake! Ole wake! (At-Tirmidhiy na amesema hii ni Hadiyth Hasan, na pia imepokelewa na Abu Daawuud)

JE VIPI MTUME (SWALLA ALLAHU ALAYHI WASALLAM) ALIKUWA AKIFANYA MZAHA

Kutoka kwa Ibn Umar (Radhiya Allaahu anhuma) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mimi nafanya mzaha lakini sisemi ila tu yaliyo ya kweli" Attwabarany

Na tukumbuke kuwa miongoni mwa alama za mnafik moja wapo anapozungumza basi husema uongo. Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Alama za munaafiq ni tatu; akizungumza husema uongo, akitoa ahadi huivunja, akiaminishwa kwa kitu hufanya khiyana" Al-Bukhaariy na Muslim.

Ndugu zangu wa kiislamu tujiepusheni na jambo hili la kusema Uongo na tuwe wenye kuwakataza na wenzetu. Na mtu anaweza kusema nitatubia lakini mara hii lazima nimpate au hii mara ya mwisho. Basi wewe waza katika akili yako na je wakati unasema uongo malaika wa kutoa roho anakuja kuchukua roho yako na hujatubia. Nini utamjibu Allah wakati umerudi kwake unasema Uongo?

ALLAH ATUJAALIE WALE WENYE KUAMBIWA MAZURI NA KUYAFANYIA KAZI NA KUKATAZWA MABAYA NA KUYAWACHA"Aaamin.

“NA KUMBUSHA, KWANI UKUMBUSHO HUWAFAA WAUMINI”(51:55).

Siri ya maisha


Huenda wengine wakakuona msafi, na huenda wengine wakakuona muovu, na huenda wengine wakakuona.......

Lakini siri ya pekee ambayo haijui mwengine ila wewe ni: 

siri ya mafungamano yako na Mungu wako

Basi wasikughuri wanaokusifu... wala wasikudhuru wanaokukejeli.......

Mwenyezi Mungu amesema: 

{Bali mtu ni shahidi juu ya nafsi yake}.

(Suratul Qiyama : 14)

Wasia tisa


Wasia tisa kutoka Quran (Suratul Hujurat) za kutufunza kudili (kuamiliana) na watu: 

1- Chunguzeni kwanza ukweli wa habari (mnapoletewa habari). 

2- Fanyeni suluhu (patanisheni baina ya watu waliogombana). 

3- Hukumuni kwa haki. 

4- Msiwadharau watu. 

5- Msitukanane kwa makabila. 

6- Msiitane kwa majina mabaya. 

7- Jiepusheni sana na kuwadhania watu dhana mbaya. 

8- Msipeleleze habari za watu. 

9- Msisengenyane

zihifadhi vizuri na uzichunge maishani. 

si jukumu lako kumfurahisha kila mtu lakini ni jukumu lako kutomuudhi mtu. 

Zingatio kwa kila mwenye mke


Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia-wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba Mtume Mohammed (s.a.w) alisema:-((Wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao))

Ushauri muhimu kwa wote


Madamu moyo wako bado unapiga, usipoteze mambo matatu:

-Imani yako kwa Mungu
-Tumaini lako kwa Mungu
-Tegemeo lako kwa Mungu

Tunafanya mambo tunavyotaka sisi, bila kuangalia wapi Mungu katoa na wapi kaharamisha, na wapi kafaradhisha...Ewe Mungu wetu tunajikinga kwako na shida mbili: (mandhari mabaya na mabadiliko mabaya). 

Huenda mauti yapo karibu nasi na hatuhisi,huenda yanakumbatia pumzi zetu kila sekunde nasi tumeghafilika! Ewe Mungu tupe nafuu wakati wa kutolewa roho na tupe mwisho mwema. 

Usiamini sana, usipende sana, usitumai sana,kwani mno itakuumiza sana. 

Toa nasaha na usifedhehi, na laumu bila kujeruhi. 

Hakuna budi kuwepo na kukinai (kuridhika) kikweli kweli kwamba tuliyoandikiwa tutayapata hata kama hatuyataki...na tusiyoandikiwa hatutayapata hata kama tutayapigania hadi kifo. 

Pale nia zinapokua safi, matamanio yetu tutayafikia. 

Mimi ni Muislamu, na Uislamu ni dini kamili; lakini mimi ni binadamu si mkamilifu..
kwa hiyo nikifanya makosa musilaumu Uislamu bali nilaumuni mimi. 

Heshima ni malezi si udhaifu, na kuomba radhi ni tabia si madhila

Usihuzunike asipothamini mtu juhudi na wema wako, kwani tabia ya watu hawadiriki neema ila baada ya kuwatoka

Ewe Mungu tupe woga ili utuzuie na kukuasi, na tupe uchamungu ili itufikishe peponi mwako, na tupe yakini ili ituwepesishie Maafa ya dunia...

Nasaha Muhimu


Anza siku yako kwa kumtaja na kumkumbuka Mungu katika nyakati za asubuhi upate kufaulu.

Endelea na kuomba msamaha kwa Mungu mpaka shetani akaribie kujiua.

Usiache dua kwani ndio kamba ya uokofu.

Kumbuka maneno yako yanaandikwa na malaika.

Kua na matarajio mema hata kama uko katika kidimbwi cha kimbunga (matatizo).

Uzuri wa vidole ni kuvifungamanisha na tasbih.

Wasiwasi na dhiki zikizidi sema: "LAA ILAHA ILLA ALLAH."

Nunua dua ya fakiri na mapenzi ya maskini kwa pesa.

Sijda ndefu kwa ajili ya Mungu yenye unyenyekevu ni bora kuliko makasri mazuri (Majumba ya kifakhari).

Fikiri kabla hujatoa neno kwani huenda neno likaua.

Jihadhari na dua ya madhlum na chozi la mwenye kunyimwa (maskini).

Kabla kusoma vitabu na magazeti: soma 
Qur-an.

Tengeza sababu ya kunyooka watu wako.

Jitahidi nafsi yako katika utiifu kwani nafsi ni yenye kuamrisha maovu sana.

Busu viganja vya wazazi wako utapata radhi.

Nguo zako kuukuu ni mpya kwa mafukara.

Usighadhibike (usikasirike) maisha ni mafupi kuliko unavyodhania.

Uko na mwenye nguvu wa wenye nguvu na tajiri wa matajiri naye ni Mungu Aliyetukuka.

Wingi wa kutoka kwako pasi na haja ni inadi na uovu.

Usifunge mlango wa kabuli kwa maasi.

Sala ni kitu bora cha kukusaidia kwenye misiba na machofu.

Jiepushe na dhana mbaya utapumzisha watu na utapumzika wewe mwenyewe pia.

Sababu ya kila dhiki ni kumpa nyongo Mungu basi mkabili (muendee).

Sali sala utakayoingia nayo kaburini mwako.

Ukimsikia asi anasengenya mwambie: mche Mwenyezi Mungu.

Dumu katika kusoma surat Tabaraka kwani inaokoa.

Mwenye kunyimwa (maskini) ni aliyenyimwa sala ya unyenyekevu na jicho la kutoa machozi.

Usimuudhi muumini.

Fanya mapenzi yako yote kwa Mungu na Mitume wake saw.

Msamehe aliyekusengenya kwani amekupa thawabu zake.

sala, kusoma Qur-an na kumkumbuka Mungu ni mafungamano ya kunawiri kifuani mwako.

Anayekumbuka joto la moto anasubiria sababu za maasi.

Madamu usiku hupita basi uchungu utaondoka, na matatizo yatatatuka na shida itapita.

Epuka kusengenya (qiila wa qaala: alisema, kulisemwa)kwani una amali kama majabali.

Sali kwa unyenyekevu kwani yote yanayokusubiri si muhimu kuliko sala.

Weke Qur-an kichwani kwako kwani kuisoma aya moja ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.

Maisha ni mazuri na kizuri zaidi ni wewe kwa imani yako na tabia yako na heshima yako.

Zingatia haya yatakusaidia katika maisha yako..

Kitu kizuri na chenye manufaa duniani ni kuilea nafsi iwe yenye kuridhika na kushukuru, na kuwa na nia safi.

Na hakuna kitu chema chenye kuleta faida kama kuwasamehe WENZAKO wote wenye kukukosea na wenye kukuchukia!

Lakin kuna jambo jingine bora zaidi hata Mtume
(S.A.W.) aliwahi kumuusia mmoja kati ya swahaba wake zaidi ya mara 3,
na kila mara alirudia akisistiza:

"USIKASIRIKE!"
"USIKASIRIKE!"
"USIKASIRIKE!"

Kwani hasira huzaa Chuki,
Chuki huzaa maudhi,
Maudhi huzaa kisirani, na
Kisirani huondosha nuru njema maishani na
huondosha mapenzi, maelewano, utulivu, na amani.

Tuazimie kutenda mema na Mungu Atatujaalia tawfiq,

In Sha Allah

Tuamrishane mema

Mtoto alimuomba mamake amueleze kwa ufupi ujuzi wake na hikma alopata maishani, mamake akwambia: "utaweza kusikiliza?"

Akajibu: ndio......

Mama akasema:

Mwanangu: jichunge na kuzungumzia watu au mambo hadi uhakikishe ukweli wake, na akikujia mtu na habari yoyote hakikisha kabla kukimbilia......!

Na jihadhari na uvumi
Usiamini kila linalosemwa, wala nusu ya unayoyaona, na Allah akikuonja kwa adui pambana naye kwa kumfanyia hisani... sukuma uovu wake kwa lililo jema, nakuapia kwa Allah uadui utageuka mapenzi...

Ukitaka kumjua undani rafiki; safiri naye!
Safarini mtu hudhihirika uhakika wa undani wake....

Watu wakikuhujuma nawe uko kwenye haki furahia; kwasababu ni kama wanasema wewe umefaulu na unaathiri, kwani mbwa akiyekufa hapigwi teke, na haupurwi ila mti unaozaa matunda....!!

Mwanangu: ukitaka kuchagua mtu... mtazame kwa jicho la nyuki na usitazame watu kwa jicho la nzi kuangalia ubaya tu ulipo!

Lala mapema mwanangu kwani baraka ya rizki ni asubuhi, nakuhofia uikose riziki ya Allah Alrahman kwa kuwa unakesha....

Na nitakuhadithia kisa cha mbuzi na mbwa mwitu ili usimuamini anayefanya hila. Na mtu akikuamini, basi chunga tena chunga usimkhuni.....!

Nitakupeleka kwenye nyumba ya simba nikuoneshe kuwa simba hakuwa mfalme wa msitu kwa kuwa ananguruma ! Lakini ni kwasababu yeye ana ezi ya nafsi, hali windo la mwenzake hata akawa na njaa sana, basi usiibe juhudi ya mwenzako ukawa dhalimu....!!

Nitakupeleka kwa kinyonga, ili uone mwenyewe hila zake.! Anajigeuza rangi kwa rangi ya sehemu aliyo, ujue katika watu pia kuna mfano wake.....!!

Jizoeshe kushukuru mwanangu.......
Mshukuru Mwenyezi Mungu inatosha kuwa wewe ni Muislamu, inatosha kuwa unatembea, unasikia, unaona,,,,,,,,,,, mshukuru Mwenyezi Mungu na uwashukuru watu.. Mwenyezi Mungu anawazidishia wenye shukrani.. na watu wanapenda wakimpa mtu ashukuru.

Sifa njema kubwa katika maisha ni UKWELI.... na jua kwamba uongo hata ukiokoa ni muovu kabisa katika sifa mbovu...

Mwanangu.... jiwekee badala ya kila kitu, jitayarishe kwa jambo lolote, ili usidhalilike na kudharaulika.

Na ufaidike na fursa yoyote unayoipata sasa, huenda usiipate tena.

Usilalamike wala usijidhalilishe !! Nataka uwe mwenye hisia chanya uyakabili maisha, wakimbie wanaokata tamaa na wenye hisia hasi... na jihadhari kukaa na mtu anayepiga bao...!!

Usifurahie msiba wa mwenzako, na jihadhari na kumdharau mtu kwa umbo lake, kwani hakuna aliyejiumba.! Na katika kufanya dharau unakuwa unamfanyie aliye umba.

Kwa mafunzo na faida.... matatu:

-Usichukue vitu vitatu mpaka uviulizie:
Asali, dini, na mke.

-na vitatu hutapumzika hadi vikuepuke:
Wasiwasi, deni, na rafiki muovu.

- na vitatu vikichelewa vinakuwa havina faida:
Walima, taaziya na sala ya maghrib.

- na watatu Mungu akulinde nao:
Mwana wa haramu, mkata kizazi, na mla riziki ya mayatima.

-na watatu jiepushe na kuandamana nao:
Aso na akili, aso jali, aso na utu.

-na watatu usiwasikize:
Muongo, mfitinishaji, na mtoa ushuhuda wa uongo.

-na watatu usiwafanye marafiki:
Hasidi, na mwenye kijicho, na mwenye kukasirisha wazazi.

-na watatu usivunje rai zao:
Mwenye kuhifadhi sala yake, na mkarimu, na mwenye kuridhisha wazazi.

TUAMRISHANE MEMA

Zingatia haya

Ndugu zangu wapendwa,

Hisani yako na utangamano wako hausahauliki, usijute kwa madakika uliyomfurahisha mtu katika maisha yake hata kama alikuwa hastahiki kufanyiwa hivyo...! Kuwa kitu kizuri katika maisha ya kila anayekujua.

Inatutosha kuwa tuna Mungu anatulipa wema kwa wema....!!!

Maisha yetu ni karatasi

Cheti cha kuzaliwa ni .....karatasi

Cheti cha chanjo ni
.....karatasi

Cheti cha kufaulu ni
..... karatasi
Cheti cha kuhitimu ni
....karatasi

....karatasi zinafatia.....

Cheti cha ndoa...karatasi

Pasi ya kusafiri...karatasi

Hati miliki ya nyumba...
Karatasi

Cheti cha tabia njema...
Karatasi

Wasifa ya matibabu...
Karatasi

Ualishi wa shughuli....
Karatasi

Maisha yetu ni karatasi kwenye karatasi......
Zinakunjwa na siku..na kupasuliwa...kisha dunia inazitupa zote...karatasi........

Mwanadamu mara ngapi anahuzunika..kwa karatasi, na kufurahika......kwa karatasi..
Lakini.........

Karatasi ya pekee ambayo mwanadamu hawezi kuiona ni:
Karatasi ya cheti cha kufariki....

Ifanyie kazi kwani ndio karatasi muhimu..!

Mkono kwa mkono hadi peponi.

Nyiradi za asubuhi na jioni

Application ya simu ‘Nyiradi za asubuhi na jioni na dua za Quran na maana yake kwa kiswahili' 

https://play.google.com/store/apps/d...m.Asmi.nyiradi

Yasome haya yatakusaidia katika maisha yako

Mueke chura kwenye kiti cha dhahabu utamuona ataruka aende kwenye tope hivi ndio baadhi ya watu walivyo, namna utakavyomuenua atarudi mahala anapotoka....

Usimhuzunikie mtu aliyekubadilikia ghafla, huenda ikawa ameacha kujifanyisha.. (pretend)

Mwenyezi Mungu amewaumba malaika wana akili bila ya matamanio, na akawaumba wanyama wana matamanio bila akili, na akamuumba mwanadamu akampa akili na matamanio, basi ambaye akili yake itashinda matamanio yake anaungana na malaika, na ambaye matamanio yake yatashinda akili yake anaungana na wanyama.

Mwanadamu maishani ni kama kalamu (pencil), anachongwa na makosa ili aandike kwa khati nzuri..anaendelea hivi mpaka kalamu iishe na kunabaki mazuri aloyaandika.

Usililie kila kitu kilichopita na iwe ni funzo kwako, hakuna kitu kinakufanya mkubwa isipokuwa maumivu makubwa, na sio kila kuanguka ndio mwisho kwani kuanguka kwa mvua ni mwanzo mwema.

Uslubu wako ni fani: kutangamana na wengine ndio cheo chako, kila uslubu wako ukipanda cheo chako kinapanda.

Wanamsifu mbwa mwitu naye ni hatari kwao, na wanamdharau mbwa naye ni mlinzi wao...watu wengi wanawadharau wanaowahudumia na wanawaheshimu wenye kuwadharau.

Kuwa na mnyama rafiki ni bora kuliko kuwa na rafiki mnyama!!

Nilitabasamu nilipokosa ninachokitaka nikafahamu kuwa Mungu anataka nipate zaidi ya ninachotaka nikatabasamu tena upya...

Ukiumia kwa maumivu ya mwengine basi wewe ni mwema, na ukishiriki katika matibabu yake, basi wewe ni mtukufu...

Huyu ndio "Shetani"

Je unaijua Kazi yake katika jamii?

"Hapendi kuona AMANI katika Ndoa",
Hataki kuona UKISALI",
Anapenda kukuona ukitafuta "PESA" Bila kuridhika!"

Je unajua anapoishi?
Sehemu anayopenda ni pale ambapo hakuna jina la Allah (sehemu ambayo hatajwi Mwenyezi Mungu)!

Vipi unawafahamu rafiki zake?

Rafiki zake wakubwa ni...!
WAZINZI, WEZI, WALEVI, WANAFIKI, WAONGO, WALA RIBA, WASIO HESHIMU WAZAZI, WASIO SWALI, na WAFITINISHAJI.

JE unaijua fimbo yake ya kumpigia?

Wewe sema AUDHUBILLAH MINASHAYTWAANRAJIIM! (Najikinga kwa Mwenyezi Mungu anilinde na Shetani)
Au wewe mtaje , MUNGU kila mara mfano, uwe unasema ALLAH AKBAR (Mungu Mkubwa kuliko kila kitu), N.K

Mimi nimefikisha ujumbe kwako je wewe unamfikishia nani?

Tupunguzeni israfu na tuwasaidie maskini

Ni mara ngapi unafanya israfu ya chakula?

Ni mara ngapi unakitupa chakula kilichobaki kwa kuwa hamkitaki wala hakijaharibika?

Ni mara ngapi ni mwenye kuwalisha wenye nacho na kuwasahau maskini na mafukara wenye kulala na njaa?

Watoto wangapi wanakufaa kwa sababu ya njaa?

Tuko wapi Ummat Muhammad? Kwa nini usijipangie kawaida ya kutoa kwa kuwa unacho au kila pale utakapopata?

Nyoyo zimejaa tamaa hatutosheki na tunavyoruzukiwa. Muislamu anatupa nguo hali ya kuwa jirani yake hana cha kuvaa au muislamu mwenzake nchi za kimaskini hana cha kukivaa?

Tukumbuke hizo ni neema kwa Allah na tutakuja kuulizwa. Au tunasubiri watokezee wakristo ndio waje kuwasaidia waislamu ?

Sayyidina Othmaan alitoa sadaka ya msafar mzima wa biashara yake kwa waislamu wenye njaa. Hivi muislamu anaweza kusema hatonunua nguo kwa sababu anazo nyingi bali atoe sadaka?

au atatamani na yeye anunue ili azidi kujifakhirisha?

Ukifa unaenda na sanda tu huendi na viatu vyako wala nguo zako tanguliza mema kwa ajili ya maisha ya akhera. Mwanamke anaweka kanga zinafika pea 100 au mwanamme anaweka kanzu au nguo nyengine tele wallah kuna watu wanahitaji mvao mmoja au nguo moja tu ili ajistiri na mjuislamu anayajua ila moyo wake haushtuki. Raha yake ajaze nguo kabatini.

Subhana Allah wapi tunakwenda enyi waislamu?

Kwa nini tusikae tukawaza mambo ya kheri?

Tufanyeni haya kwa ajili ya Allah na si kujionesha.

Tukumbukeni aya za Allah zifuatazo :

"Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema." (8:102)

"Ogopeni Siku Ambayo Mutarudishwa Kwa Allah Kisha Kila Nafsi Italipa Kila Lile Ililochuma Na Wao Hawatadhulumiwa"(2:281)

Mtume Muhammad s.a.w anatwambia katika hadith refu ilopokelewa na Imamu Muslim, kua mja ataambiwa na Allah "Ewe mja wangu nilikutaka unilishe lakini hukunilisha, Mja atasema vipi nitakulisha hali ya kua wewe ndie Mola wa viumbe vyote?

Allah atamuambia;Jee hukujua kua mja fulani alihitaji umlishe lakini hukumlisha? Jee hujajua kama ungelimlisha basi ungelilikuta hilo kwangu?"

Nitakutumieni video yenye kutoa chozi juu ya misiba iliyowahi kuwakuta somalia. Halafu tuseme na nafsi zetu juu ya hali hizo.

Zingatia haya na yatumie katika maisha yako yatakusaidia

"Mtu aliyezama kwenye mapenzi ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka,,,,,,,,

,,,,, namna anavyo chapwa na mitihani ndivyo anavyozidi mapenzi na kujikaribisha kwa Mungu"

Ameangamia kila anayeadhibu na kukhini na kudharau hisia za mwanadamu, hajui kuwa katika ulimwengu huu.... unavyowatendea watu ndivyo utakavyolipwa.

Ni uzuri ulioje uvae tabia njema zako.... na ujitie manukato ya tabasamu lako.. hata yanapokua.. mandhari (shepu) yako.... ni ya kiajabu na kutofahamika kwa wengine.... utakuta kizuizi hiki kinafifia na utafurahia.......

Mke hana haja ya.....
matumizi na maskani (nyumba) peke yake.... lakini pia... anahitaji maneno mazuri, moyo mzuri, mapenzi.. na huruma... mhurumie mke wako na msahaulishe mchoko wake......

Baadhi ya watu, ukiwaheshimu,.... wanazidisha kukutendea uovu,.... (wewe usijali usiaje kuwa mwadilifu)

Urafiki mwema: ni ule..... unaokufanya ukaishi maisha mawili...,

moja hapa... ingine .... peponi.........


Kujiheshimu..., heshima sio katika mavazi peke yake.... bali kuna kicheko...cha kuheshimika... mwendo wa kuheshimika..... na tabia za kuheshimika..........

Usimuache mtu mpenzi (muhimu) kwako kwasababu ya kosa (kuteleza).....au ila aliyonayo.... hakuna aliye kamili... isipokuwa Mwenyezi Mungu... Utukufu ni wake Yeye tu......

Katika matatizo ya watu....wanaweza kufuta... historia yako nzuri yote.... kwa ajili ya msimamo wa mwisho ambao haukuwapendeza.....

Uzuri hauna thamani.......bila fikra...na maadili mema....na tabia.

Haupimwi utamu wa mwanadamu...kwa utamu wa ulimi.... ni maneno mangapi mazuri...yameficha sumu ya nyoka..... kwani tupo katika wakati... mambo yamevurugika...

Peaneni msamaha.... na muzifanye nyoyo zenu nyeupe..... na kumbukeni kuna siku...... hatutakuwa katika maisha haya....

Vitu vyote vinaenda havirudi..... isipokuwa dua.....inaenda na matumaini: ....na inarudi [na zawadi].

Maneno ni kama dawa.... machache yake yanufaisha ..... na mengi yanaua....

Urafiki si....kubaki na rafiki...muda mrefu..., .........urafiki ni kudumu ...... kwenye ahadi ikiwa....ni masafa marefu au mafupi....

Katika ajabu ya mwabaadamu...anakimbia anaposikia (nasaha) na anaskiza anaposikia (fedheha)

Kuna watu wanahitaji ........ urekebishaji wa kupambwa kindani.... kukuzwa moyo, ... kuondolewa chuki..... kukazanishwa ulegevu wao wa fikra..., kuvunjwa chembe chembe (cells) za shari kwenye nafsi zao..... na kupulizwa dhamiri zao dhaifu.....


Ulimi ni mhalifu!.... mfungwa nyuma ya meno!.... ukiufungua wakati wa hasira... utakutupa kwenye kipango cha majuto ".....
...... chini ya hukumu.... ya dhamiri !

Hebu jiulize masuala haya.....

HEBU jiulize masuala haya na lifikirie katika akili yako kila suala jibu utapata mwenyewe 
Mimi ni nani katika hii dunia?

Nimeishi miaka mingapi hadi sasa?

Nimebakiza miaka mingapi ya kuishi?

Nimefanya mangapi kwa ajili ya akhera yangu?

Maovu mangapi nimetenda kwa kuteleza au kwa makusudi?

Lini nilitoa chozi kutubu mabaya yangu? 

Lini nilikaa faragha na kumshukuru M/Mungu kwa wema anaonitendea? 

Hivi Mungu akichukua roho yangu wakati huu, nimebeba kazi (amali) ngapi za kheri zitakazo nisaidia?.

Nitakumbukwa kwa wema gani niliowatendea wanadamu na viumbe wengine?

ZINDUKA NDUGU YANGU.DUNIA ISITUHADAE TUKAMSAHAU MUNGU. Wakumbushe na wengine.